Rais Shirikisho la soka nchini TFF , Jamal Malinzi ametuma salamu za pongeza kwa Hani Abou-Reida kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais Mpya wa Shirikisho la soka la Misri (EFA) katika uchaguzu mkuu uliofanyika juzi Jumanne Agosti 30, 2016 jijini Cairo.

Katika salamu zake, Rais Malinzi ameelezea kuwa kuchaguliwa kwa Hani Abou-Reida katika wadhifa huo ni kilelelezo cha familia ya mpira wa miguu ya Misri kuona umuhimu wake katika kutumikia shirikishi hilo sambamba na kuwa mwakilishi FIFA.

Rais Malinzi amesema ana imani na Abou-Reida kuwa ataweza kutumikia vema nafasi hiyo sambamba na kutumikia wadhifa wa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Kimataifa la soka  (FIFA).

Image result for Hani Abou-Reida in SoccerHani Abou-Reida

Abou-Reida (63) ni mjumbe wa FIFA kutoka Kanda ya Afrika Kaskazini tangu mwaka 2009 na sasa ataongoza shirikisho la EFA kwa awamu ya kwanza kwa miaka minne ijayo akichukua nafasi ya Galam Allam aliyeongoza EFA tangu mwaka 2012.

Katika uchaguzi huo, wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa EFA waliochaguliwa ni pamoja na wale wenye majina maarufu kama vile Hazem Emam ambaye alikuwa nyota mahiri wa klabu ya Zamalek sambamba na kiungo mkabaji mahiri wa zamani wa klabu ya Al- Ahly. Nyota hao pia walipata kuchezea timu ya taifa maarufu kwa jina la Pharaohs.

Pia wamo Sahar El-Hawary, Hazem El-Hawary, Karam Kordi, Khaled Latif, Seif Zaher, Mohammed Aboud El-Wafa, Ahmed Megahed a Essam Abdel-Fatah.

Semina Ya Klabu Za Wanawake Ligi Kuu
Sebastian Nkoma Kuongoza Benchi La Ufundi La Kilimanjaro Queens