Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu imetupilia mbali ombi la Mawakili wa aliekua rais wa TFF Jamal Malinzi la kutaka Mkurugenzi wa Mashtaka DDP afike Mahakmani kueleza sababu za kuchelewa kwa jalada la kesi yao.

Upande wa utetezi katika kesi ya kutakatisha fedha inayomkabili Rais wa zamani wa TFF Jamal Malinzi na katibu wake Mwesigwa walitoa ombi la kuitaka Mahakama imuite Mkurugenzi wa mashktaka DPP aje kueleza kwanini jalada la kesi yao limekwama katika ofisi yake.

Akitoa uamuzi wa ombi hilo Hakimu Wilbroad Mashauri amesema hakuna haja ya DPP kufika mahakamani kwani majibu yanayotolewa na Mawakili wa Serikali ndo hayo hayo yatatolewa na DPP.

Hakimu Mashauri amesema mawakili wa Serikali wanafanya kazi na DPP hivyo hata DPP akija Mahakamani hatokua na jipya.

Kesi hiyo imeaghirishwa hadi November 17 na watuhumiwa wote wamerejeshwa rumande.

Malinzi na Mwesigwa wanakabiliwa na makosa mbali mbali ikiwemo kosa LA kutakatisha fedha.

Nayo kesi ya kutakatisha fedha inayowakabili Rais wa klabu ya Simba Evance  Aveva na Makamu wake Geoffrey Nyange Kaburu imetajwa Ijumaa hii.

Upande wa mashtaka umeileza Mahakama kuwa jalada bado lipo kwa DPP.

Kesi hiyo pia imeaghirishwa hadi November 17  mwaka huu.

Aveva na Kaburu wanatumuhumiwa kwa makosa matano ikiwemo kughushi nyaraka na kutakatisha fedha.

Video: Nape aikosoa vikali miradi ya JPM
Papa Francis apiga marufuku uvutaji wa sigara Vatican