Mwanamuziki nyota wa Bongo flava ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa WCB, Diamond Platnumz amedokeza kwamba msanii aliye chini ya label yake Zuchu atalazimika kulipa kiasi cha pesa kisichopungua Shilingi 10 Bilioni ikiwa atahitaji kujitoa lebo hiyo.
Nyota huyo, ameweka wazi kuwa kiwango cha msanii Zuchu kimekuwa kwa kiasi kikubwa na kwamba jambo hilo ni matokeo ya uwekezaji mkubwa, alioufanya na ndio sababu ya kutaja thamani hiyo ya fedha.
Haya yanajiri, ikiwa ni wiki chache baada ya kuenea kwa tetesi kuwa Diamond anawanyonya wasanii walio chini ya WCB, na kuwafanya kulipa kiasi kikubwa cha fedha ili kukatisha mikataba yao.
Hata hivyo, Diamond alisema record label hiyo inawekeza fedha nyingi kwa wasani inaongia nao makubaliano ya kikazi, ili kuwarahisishia kupata umaarufu ndani ya muda mfupi, kitu kinachowalazimu kulipa kiasi kikubwa cha fedha ikiwa wana nia ya kuondoka.
Amesema, “Huwezi kuondoka tu wakati tumewekeza mamilioni kwako. Nawekeza kwa watu, nahakikisha wanakuwa na jina kubwa, pamoja na matamasha ili mwisho wa siku tupate pesa.”
Diamond ameongeza kuwa, “Ningeweza kuwekeza pesa hizo katika kitu kingine, lakini ninachagua kuwekeza katika burudani na Wasanii wa WCB ni matajiri kwa sasa kutokana na uwekezaji tunaoweka kwao.”