Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amelazimika kuusimamisha uongozi wa  Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kujibu kero mbalimbali baada ya kuwasikiliza wananchi wa kijiji cha Isangati Kata ya Iyunga Mapinduzi waliotaka ufumbuzi wa matatizo yao kwa Serikali.

Malisa amezungumza na wananchi hao kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mpira wa kijiji cha Isangati, wenye lengo la kuhamasisha mapokezi ya mwenge unaotarajia kuwasili Agosti 10, 2023 katika uwanja huo.

Katika Mkutano huo, wananchi walieleza kero mb za maji, shule, umeme, barabara, ufungwaji wa mipaka ambayo huwasababishia kushuka kwa bei ya mazao pamoja  na kipimo cha ujazo wa gunia la viazi kuzidishwa.

Kufuatia kero hizo, DC Malisa aliwainua wataalam kutoka Halmashauri hiyo na kujibu baadhi ya kero hizo, kisha mwenyeketi wa Halmashauri Mwalingo Kisemba  kufanya majumuisho ya kutolea ufafanuzi zaidi changamoto hizo.

Singida Fountain Gate kujipima Kenya, Uganda
Kamwe amtaja Namba 06 Young Africans