Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amewataka wahitimu wa kada mbalimbali za afya katika taasisi ya Sayansi za Afya Mbalizi kufanya kazi kwa uaminifu pindi watakapopata nafasi za ajira.

Malisa katika Mahafali ya 19 ya Taasisi ya Sayansi za Afya Mbalizi, yaliofanyika katika hoteli ya Ifisi, iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Mkoani Mbeya, akiwa mgeni rasmi kumuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa.

Amesema, “jambo kubwa katika soko la ajira ni utayari wao wa kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu na uzalendo kwani Tanzania ni nchi kubwa na inauhitaji mkubwa wa wataalamu wa afya na ninyi ndio wahitimu katika mahafali haya.”

Hata hivyo, Malisa amesema Serikali ya awamu ya sita imetoa fursa lukuki kwa wataalamu wa afya na hivi karibuni kwa uwepo wa ajira nyingi, hivyo anaamini wahitimu hao wako tayari na wana uzalendo wakutosha na endapo watapata ajira wafanye kazi kwa uaminifu.

Zifuatazo ni baadhi ya Picha za kumbukumbu wakati wa mahafali hayo.

Magonjwa yasiyoambukizwa yaundiwa mkakati
Ihefu FC wameanza mdogo mdogo Mbeya