Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amewataka Walimu kuitumia fursa ya uanzishwaji wa Kifurushi cha Mwalimu Spesho, kinacholenga kutatua changamoto mbalimbali zao, ikiwemo huduma za akiba na amana kwa ajili ya uwekezaji.
Malisa aliyasema hayo kwenye Semina ya kuwajengea uelewa Walimu wa Mkoani Mbeya juu ya umuhimu wa kifurushi hicho, akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Zuberi Homera ambae yuko kwenye utekelezaji wa majukumu mengine ya Kiserikali.
Awali, Meneja Mwandamizi Wateja Binafsi wa NMB, Ally Ngingite alieleza namna ambavyo kifurushi hicho kimewasaidia Walimu wengi nchini kujieneleza kiuchumi, akisema hata hivyo kilichoanzishwa rasmi mapema mwaka jana 2022.
Huduma hiyo iliyoanzishwa na Benki ya NMB, pia inalenga kuwawezesha wateja kujiwekea amana na akiba kwa ajili ya malengo ya baadae, ili kuwainua kiuchumi.
Zifuatazo ni picha za baadhi ya matukio wakati wa Semina hiyo, iliyofanyika jijini Mbeya.