Malkia wa Uholanzi, Maxima leo (Oktoba 19, 2022), anahitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu iliyoanza Oktoba 17, 2022 baada ya kuwasili Jijini Dar es Salaam, akitokea mkoani Kilimanjaro.

Baada ya Malkia Maxima, kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), alipokelewa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Robert Kahendaguza.

Maxima ambaye pia ni Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), katika masuala ya Mfumo Jumuishi wa Fedha wa maendeleo, anatarajia kufanya mazungumzo na Rais, Samia Suluhu Hassan hii leo Oktoba 19, 2022.

Mbali na kukutana na Rais Samia pia Malkia Maxima kabla ya kuhitimisha ziara yake hapa nchini, anatarajia kukutana na viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali.

Serengeti Girls kuivaa Colombia Robo Fainali
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Octoba 19, 2022