Mwanamke mmoja nchini Mali amejifungua watoto tisa katika hali ambayo sio ya kawaida.

Katika taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mali Fanta Siby, alisema Halima Cisse, 25, alijifungua kupitia njia ya upasuaji watoto wa kike watano na wavulana wanne katika hospitali ya Morocco siku ya Jumanne ambako alikuwa amelazwa.

Cisse amekuwa akitarajia kujifungua watoto saba kulingana na uchunguzi wa skani ya tumbo aliyofanyiwa nchini Mali na Morocco lakini skani hiyo haikugundua amebeba watoto wengine wawili.

Siku ya Jumanne, Dkt Siby alisema watoto hao na mama yao wanaendelea vyema na wanatarajiwa kurejea nyumbani wiki chache zijazo.

Siby amewapongeza madaktari waliomhudumia Mali na Morocco, “ambao ujuzi wao ni chanzo cha matokeo mema ya ujauzito huu”.

Shirika la habari la Reuters limeipoti kuwa Mimba ya Cisse imeshangaza taifa hilo la Afrika Magharibi na imewavutia baadhi ya wakuu wa nchi hiyo, huku baadhi yao wakisafiri hadi Morocco alipohitaji utunzi wa kitaalamu.

Msemaji wa Wizara ya afya ya Morocco, Rachid Koudhari, ameliambia shirika la habari ya AFP kwamba hakujua uzazi wa aina hiyo hutokea nchini humo.

Samia: Watoto tunzeni wazee
Kongamano la Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kufanyika Mei 21, 2021