Bosi wa WCB, Diamond Platinumz ameonesha kwa vitendo kuwa biashara yake ya Radio na Televisheni ni kwa ajili ya wote bila kujali uhusiano wake binafsi na msanii anayetajwa.

Jana, alichukua nafasi ya kuwa mtangazaji na mcheza santuri (DVJ) wa kipindi kimojawapo akiwataka watazamaji kuchagua nyimbo wazipendazo na yeye alizitendea haki akifuata matakwa ya watazamaji.

Akionesha moja kwa moja kupitia ‘Insta Live’ akiwa ndani ya Wasafi TV, alikutana na shabiki wa Harmonize, Mama Dangote ambaye ni mama yake mzazi aliyeomba wimbo mpya wa mwanafamilia huyo wa zamani wa WCB ambaye amejitoa na kuanzisha ‘Konde Gang’.

Hata hivyo, Diamond alishindwa kucheza wimbo huo akitoa maelezo kuwa hauna video hadi sasa lakini alimpa mtazamaji ladha nyingine kutoka kwa Harmonize, ‘Shulala’ aliyomshirikisha Korede Bello.

Alisoma ujumbe mwingine wa shabiki aliyeomba wimbo wa Ali Kiba, ‘Aje’  na mwingine aliomba wimbo wa Rich Mavoco ‘Kokoro’.

Ingawa baadhi ya watu wanahisia kuwa hana maelewano mazuri na wasanii hao, alizicheza nyimbo hizo akisisitiza kauli mbiu ya kituo hicho cha TV, ‘Hii ni Yetu Sote’.

Mavoko alijitenga na WCB akilalamikia kuwa mkataba aliokuwa ameingia nao ni haukuwa unamtendea haki. Kadhalika, Harmonize juzi ameeleza kuwa ilimbidi auze nyumba zake tatu kukamilisha vigezo vya kuvunja mkataba wa WCB ambapo alitakiwa kulipa Sh. 500 milioni.

Maelfu waandamana Zimbabwe kupinga vikwazo vya Marekani, Umoja wa Ulaya
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 26, 2019