Baada ya muigizaji wa filamu na muimbaji wa nyimbo za injili, Muna love kukanusha tuhuma za kuwa na mtoto mwingine kupitia ukurasa wake wa instagram mama yake mzazi, Bi Rabia Ally Moyo amefunguka kinagaubaga na kuanika kuwa mwanaye Rose ambaye anatambulika kama Muna Love ni kweli  ana mtoto mwingine anayejulikana kwa jina la Brian ambaye ni wa kwanza kuzaliwa na yupo mkoani kilimanjaro, Wilayani Moshi kijiji cha Kahe.

Mama mzazi wa Muna amesema kuwa Muna amekuwa akificha siri hiyo na amekuwa akimkataza mama yake kuzungumza juu ya mtoto wake Brian ambaye amemtelekeza huko kijijini akidai kuwa hana mtoto mwingine zaidi ya Patrick.

”Kweli mimi kwa Rose, Rose amezaa mara mbili na mara zote amezaa watoto wa kiume wa kwanza anitwa Brian na baba yake anaitwa Fred, na wanakaa Moshi kijiji cha Kahe huyo ni mtoto wake amaezaa mwenyewe, kabla hajaolewa na baba Patrick ambaye anaitwa Peter.

Muna amefikia hatua ya kumuua mama yake kutokana na ukaribu alaiokuwa nao na mjuu wake Brian ambaye yupo Moshi kijijini.

”Likizo mimi ndiyo namfuata mtoto anaumwa mimi ndiyo naenda kumfata mjukuu wangu lakini anasema nisiseme kama huyo ni mtoto wake” amesema Bi Moyo.

Bi Moyo alizungumza hayo pindi alipofanya mahojiano na Global Tv nyumbani kwake, aidha ametangaza kuwa yeye ni mama mzazi wa Muna japokuwa Muna amekuwa akitangaza kuwa mama yake amefariki dunia na amekuwa akitanagaza hivyo kutokana na mama yake kukataa kumfichia siri ya huyo mtoto mwingine.

”Mimi ni mama wa Muna sijafa japo yeye ameniua ila mimi sijafa yeye ni mwanangu wa nne kati ya watoto wangu watano ni kweli amezaa mara mbili wa kwanza ni Brian yupo moshi hizo picha zinazozagaa kwenye magazeti ni kweli”. Bi Moyo.

Makontena ya Makonda yakosa mteja tena
Lil Wayne akiri kujipiga risasi kifuani alipokatazwa kuimba