Mama mzazi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Aprili 10, 2021 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu.
Taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi imeeleza kuwa msiba wa Monica Nyabyamani upo nyumbani kwa IGP Sirro, Masaki Dar es Salaam karibu na kwa Hayati Benjamin Mkapa.
Taratibu za mazishi zinaendelea kufanyika nyumbani kwa marehemu katika Kijiji cha Kiabakari, wilayani Butiama mkoani Mara.