Spika wa Bunge, Job Ndugai amebainisha kuwa Serikali itasimamia mazishi ya Mchingaji dkt.Getrude Rwakatare ambayo washiriki hawatazidi 10 na kuliomba Bunge kutoa ushirikiano kwa namna Serikali itakavyoelekeza.
Amesema utaratibu huo umefikiwa baada ya familia ya marehemu mchungaji kuomba mambo mawili Serikalini kuwa mama yao azikwe kwenye eneo la Kanisa la Mlima wa Moto na pia iwe Alhamis, Aprili 23.
“ Familia imeomba Askofu Rwakatare azikwe kwenye eneo la Kanisa la Mlima wa Moto, na wameomba sana mazishi yawe keshokutwa Aprili 23,2020.”
” Serikali ndiyo itasimamia mazishi hayo ambayo washiriki wa mazishi hayo hawatozidi 10” amesema Spika Ndugai alipokua akitoa taarifa kwa Wabunge juu ya maziko ya Mbunge wa Viti Maalum, Askofu Dk. Getrude Rwakatare.
Mtoto wake, Mutta Rwakatare amesema mama yake alifariki alfajiri ya jana Aprili 20, 2020 katika hospitali ya Rabininsia Jijini Dar na alikuwa alisumbuliwa na matatizo ya moyo na Shinikizo la Damu.