Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kuwa hana nia ya kugombea nafasi ya uongozi kwa ngazi ya Urais Visiwani Zanzibar.

Ameyasema hayo Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa sherehe za kimila ya Wakizimkazi, ambazo hufanyika kila mwaka visiwani humo kwa lengo la kukuza na kudumisha mila na tamaduni za wakazi wake.

”Nataka kusema kwamba kuna maneno maneno kwamba Mama Samia Suluhu anataka kugombea Urais Zanzibar, nataka kuwaambia sio kweli na sina nia hiyo, ukiangalia ngazi ya uongozi ndani ya Tanzania mimi ni namba mbili sina kishawishi chochote kinachonivuta kunileta huku niwe namba tatu sina,” amesema Mama Samia.

Amesema kuwa ameona alizungumzie suala hilo huko huko visiwani Zanzibar maana ndiko lilipoanzia kwasababu maneno yamekuwa mengi, chuki, ufisadi na majungu.

Hivi karibuni kumekuwa na maneno yanayosambazwa hasa visiwani Zanzibar kuwa Mama Samia ana nia ya kugombea nafasi ya Urais visiwani humo.

 

Anayedaiwa kumuua mkewe adai simu zake
Makonda aeleza sababu za yeye kuwa RC Dar