Mama aliyejipatia maarufu kwa kutoa nasaha zake kwa jamii kuhusu mambo mbalimbali hususan uhusiano wa mapenzi pamoja na Ukimwi, ameweka wazi jinsi anavyoingiza mamilioni ya shilingi za Tanzania kwa kutoa elimu ya ‘Ngono’ (Ngono-ology).

Akiongea jana katika utoaji tuzo za kutambua juhudi za wanawake waliotumia fursa na kujikwamua kiuchumi za ‘Malkia wa Nguvu’ zilizoratibiwa na Clouds Media huku Mgeni rasmi akiwa Spika wa Bunge la Kumi, Anne Makinda, Mama Terry alisema kuwa aliamua kuitumia elimu ya masuala ya Ngono baada ya rafiki yake mmoja kumwambia kuwa anastahili kuwa na shahada ya Uzamivu ya masuala ya Ngono (PhD in Ngono-ology).

Alisema hivi sasa anafanya kazi ya kuelimisha kuhusu ‘ngono-ology’ nchini Nigeria ambapo kwa jiji la Abuja pekee anaingiza shilingi milioni 30 kila baada ya wiki tatu kwa kutoa huduma hiyo.

“Hivi sasa nataka kuongeza mtandao naenda jijini Lagos na sehemu nyingine,” Mama Terry alisema.

Akiongea mbele ya umati mkubwa uliohudhuria tukio hilo la lililotanguliwa na utoaji mada kwa lengo la kuzitambua fursa ambazo wanawake wa Tanzania wanaweza kuzitumia, alisema kuwa nchini Nigeria bado kuna fursa nyingi za kiuchumi ambazo watanzania wanaweza kuzitumia kwakuwa wakati shanga moja huuzwa shilingi 5,000 hapa nchini, Nigeria inapauzwa shilingi 200,000.

Takukuru waanza kuchunguza sakata la Rushwa kwa Lukuvi
Rais Magufuli ateua Wakuu wa Mikoa wapya, Makonda aikwaa Dar