Mwimbaji wa RnB Chris Brown, amelazimika kusitisha malipo ya $10,000 kila mwezi kwa mzazi mwenzake Nia Guzman kama pesa ya matunzo ya mtoto wake Royalty baada ya kugundua kuwa mtoto huyo alipelekwa kwa bibi yake (mama Chris Brown) huku yeye akikataliwa kumchukua.

Chris ambaye amekuwa katika hali ya kugombana na kuelewana na mama yake, Joyce Hawkins kwa miaka mingi alichukua uamuzi huo kwa hasira kwa kuwa alikuwa na mpango wa kumtembelea mama mtoto wake na kumchukua Royalty kwa kipindi cha wiki moja lakini alikataliwa kabla ya kugundua kuwa mtoto huyo alimpelekwa kwa bibi yake kwa siri.

Kwa mujibu wa TMZ, Chris amepeleka maombi mahakamani akimtaka jaji kuwasaidia kumaliza mgogoro wao wa matunzo ya mtoto huyo.

Boko Haram Waua Waumini 150 Msikitini
Blatter: Nitakapoingia Peponi Ndipo Mtaamini Sikutafuna Rushwa