Rais wa Colombia, Gustavo Petro, amesenma kwamba mama mzazi wa mchezaji wa Colombia na klabu ya Liverpool ya England, Luis Diaz, aliokolewa juzi Jumamosi (Oktoba 28) baada ya kutekwa nyara kaskazini mwa nchi hiyo, lakini maofisa wanaendelea kumtafuta baba yake aliyetoweka.

Ofisi ya mwanasheria mkuu wa Colombia hapo awali ilisema ilikusanya timu ya wachunguzi kuwatafuta wanandoa hao huko Barrancas, manispaa ya jimbo la kaskazini mwa Colombia la La Guajira.

Polisi walithibitisha kuokolewa kwa mamaye Diaz, Cilenis Marulanda, na kusema alizungumza na Mkurugenzi William Rene Salamanca. Katika video, Salamanca alisema anatumia kila namna kumtafuta baba yake Diaz.

Wazazi wa Diaz mwenye umri wa miaka 26, waliripotiwa kutekwa nyara walipokuwa wakiendesha gari kuelekea nyumbani kwao.

Watu wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki waliwasimamisha na kuwashusha kwenye gari, mamlaka ilisema.

Shirikisho la Soka nchini Colombia lilisema katika taarifa yake kwamba utekaji nyara huo ni wa kusikitisha na kuwataka viongozi kumwokoa baba huyo.

Try Again: Ihefu FC imetupa mazoezi ya Dabi
Pacome. Aziz Ki wazusha hofu Avic Town