Beki wa zamani wa Liverpool, Mamadou Sakho anakabiliwa na tishio la kufutwa kazi huko Montpellier baada ya kudaiwa kumshambulia kocha wake, Michel Der Zakarian wakiwa mazoezini.
Ripoti kutoka Ufaransa zinadai kuwa Sakho, ambaye alichezea Liverpool na Crystal Palace katika Ligi Kuu ya Uingereza, alijibizana vikali na bosi wake.
Inasemckana beki huyo mwenye umri wa miaka 33 alimshika Der Zakarian kwenye kola na kumwangusha chini.
Kisa hicho kinachodaiwa kilitokea mbele ya mashahidi kadhaa kilizuka baada ya Der Zakarian kumkashifu Sakho wakati wa mazoezi.
Inaaminika Montpellicr inazingatia mikataba yao, ikiwa ni pamoja na kusitisha ajira ya mchezaji huyo, japokuwa Sakho na Der Zakarian walizungumzia sakata hilo.