Miongoni mwa ndege anayefugika katika jamii zetu ni kuku, ambaye pia ni kitoweo pendwa cha wengi. Lakini yapo mambo mengi na ya kustaajabisha kuhusu maisha ya ndege huyu. Kwa mujibu wa Jarida la Wanyama na Ndege la Uingereza toleo la 2018, yafuatayo ni kati ya mambo yakustaajabisha yanayomhusu ndege huyu

  1. Kuna idadi kubwa ya kuku duniani kuliko idadi ya binadamu. Kwa makadirio kuna kuku zaidi ya bilioni 25. Pia, kuku ndio ndege wengi zaidi duniani katika kundi ya kisayansi la familia ya ndege.
  2. Kuku wana uwezo wa kukumbuka zaidi ya sura 100 za watu na wanyama.
  3. Kuku tetea anayeatamia hugeuza mayai yake mara 50 kwa siku na ana uwezo wa kuatamia mayai 300 kwa mwaka.
  4. Rangi ya mayai ya kuku yanategemea rangi ya masikio yake. Kuku mwenye masikio yenye rangi nyekundu hutaga mayai ya ‘brown’ (kahawia) na kuku mwenye masikio meupe hutaga mayai meupe.
  5. Kuku wana uwezo wa kuhisi chumvi kwenye chakula lakini hawawezi kuhisi sukari kwenye chakula.
  6. Kwa wastani, kuku 97 huchichwa duniani katika kila baada ya sekunde 0.05.
  7. Kuku akitenganishwa kiwiliwili na kichwa anaweza kurukaruka umbali wa ukubwa wa uwanja wa mpira.
  8. Mwili wa kuku una asilimia 15 ya maji zaidi ya mwili wa binadamu.
  9. Njia yao ya kipekee ya kuwasiliana ni milio ambayo wanayo zaidi ya 30.
  10. Kuku hujisafisha kwakutumia vumbi, huchimba shimo dogo na kujigeuza geuza kwenye vumbi la shimo hilo hadi watakapo lidhika, kisha hutoka na kujikung’uta.

 

 

 

Umoja wa Mataifa waipongeza Tanzania kwa hili
Nash Mc afunguka kuhusu wasanii kutojikubali