- Kupungua kwa kiwango cha mkojo
Kiafya mtu anatakiwa kwa wastani akojoe mara 6 hadi saba kwa siku. Kama unakojoa chini ya mara mbili kwa siku basi gundua hunywi maji ya kutosha.
- Ngozi kuwa kavu sana
Ukiona una ngozi kavu basi tambua huna maji ya kutosha mwilini kwani ata kiwango cha maji kwenye ngozi yako inatokana na unywaji wako wa maji..
- Kuumwa kichwa
Ukiona unasumbuliwa sana na kichwa basi tambua kichwa hicho kinawezekana kua ni sababu ya upungufu wa maji.
- Mdomo mkavu
Ukosefu wa mate na mdomo kuwa mkavu hiyo husababishwa na upungufu wa maji.
- Rangi ya mkojo
Rangi ya mkojo inatakiwa iwe nyeupe ikiwa na unjano kwa mbali kama unakunywa maji ya kutosha. Kama ukiona rangi ya mkojo si ya kawaida kuwa njano kupitiliza basi tambua una upungufu wa maji mwilini.
Zifahamu Mbinu Chafu Na Sababu Za Rafiki Msaliti Kumchukua Mpenzi Wako
Hata hivyo Dkt. Thomas Mboya kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili amesema kuwa mbali na dalili izo pia kuna dalili nyingine kama mtu kupata kizunguzungu, kutotokwa na jasho hata kipindi cha joto, kutokwa na haja kubwa ngumu na ngozi kujikunja.
Naye Dkt. Mariam Maroa kutoka hospitali ya wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam anasema maji ni umuhimu katika mwili wa binadamu kama vile kusaidia katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, mfumo wa damu, na kuweka hali ya jotomwili sawa.
Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UNICEF, watu bilioni 1.1 hawana uwezo wa kupata maji safi duniani. Hii inaweza kuwa sababu ya watu kutokunywa maji kwa kiwango kilichowekwa kwa mujibu wa afya.
Kunywa maji kwa Afya.