Kuna namna ambayo mtu anaweza kufanya ikaleta tafsiri ya mtu huyo kuonekana mwenye akili lakini pia kuna namna ambayo mtu anaweza kufanya jambo ikamletea tafsiri kuwa mtu huyo hana akili, kutokuwa na akili haimanishi kuwa ni kichaa lakini unaweza kuwa ni mtu mzima tu lakini ukaonekana akili zako hazijajitosheleza.
Mara nyingi watu wenye akili hutambulika kwa mambo mengi, ikiwemo namna anavyofikiria na kufanya maamuzi, maendeleo yake, namna ambavyo anaweza kutatua changamoto kwa uharaka na usahihi, lakini pia namna ambavyo anaweza kuwa msaada kwa wengine.
Binadamu huzaliwa na akili lakini kiwango cha akili kwa mtu mmoja na mwingine hutofautiana kutokana na sababu nyingi, japokuwa kisayansi sababu huanzia huanzia tangu pale mimba inapotungwa hadi mtoto anapozaliwa.
Akili zinaweza kurithiwa au kupatikana kutokana na mazingira pamoja na maishi unayoishi, kwa mujibu wa wataalamu, mazingira yanayokuzunguka yanaweza kuathiri uwezo wa ubongo wako na namna ambayo unafikiria, na kuchukua maamuzi katika maisha unayoishi.
Hata hivyo kwa mujibu wa wataalamu wamebaini kuwa watu wote wenye akili huwa na tabia zinazofanana na pia huwa na vitu vingi vinavyoendana.
Taarifa zilizokusanywa na watafiti, Bright Side wamechambua mambo 9 ambayo watu wenye akili huyafanya kama ifuatavyo
- Hawapendi kufanya umbea, tafiti zinaonesha wanapenda kuwa wapweke japokuwa haimaanishi kuwa ni wapweke (loners) bali wanapenda kupata nafasi ya kufikiria zaidi.
- Wanapenda kuchekesha/kufurahisha watu wengine, wana uwezo mkubwa wa kugeuza jambo lolote na kuwa la kufurahisha.
- Wanapenda kuongea wenyewe, mwanasayansi Albert Einstein alikuwa na tabia ya kuongea mwenyewe.
- Wanapenda kusikiliza muziki mara nyingi, wanapenda kuwa na spika za masikioni (Earphones) muda wote, inaelezwa pia wanapenda kusikiliza nyimbo zisizo eleweka wanapendelea kusikiliza biti kuliko mashairi.
- Hufanya kazi kwa umakini na sio kutumia nguvu kubwa, wana tabia za uvivu na hiyo ndio huwafanya kupenda kutaka kurahisisha vitu mbalimbali.
- Wanapenda kujifunza na kutafuta majibu ya kila changamoto wanayokumbana nayo, hupenda kusoma sana vitabu na kuwela kumbukumbu ya mambo yao katika diary.
- Wanakubali kirahis pale wanapoona wamekosa
- Wanapenda kula sana chokoleti
- Hawapendi kuongea sana, wanapenda kuongea pale wanapoona inafaa kwa muda huo, endapo kutatokea majibizano hawapendi kujihusisha nayo.