Baada ya Kufanya mikutano ya kampeni kwa wiki mbili mgombea nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ,Tundu Lissu ametoa tasmini na mwenendo wa kampeni katika kanda 10 za chama hicho .

Akizungumza na wahariri na wandishi wa habari nyumbani kwake leo ,amesema kuwa chama chake akiwezi kujidanganaya juu ya ugumu wa kazi ya  kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 2020.

“Hakuna ambaye anajidanganya, kazi iliyopo mbele yetu ni kubwa kwelikweli, mimi binafsi nimeshiriki hizi chaguzi za Tanzania ya vyama vingi tangu 1995, ninafahamu jinsi uchaguzi wa Tanzania ulivyo mgumu kwa chama chochote cha upinzani” amesema Lissu .

Lissu amesema kuwa uchaguzi mkuu huu ni muhimu kuliko chaguzi zilizopita kwa sababu kunauwezekano wa chama chake kuingia madarakani.

Zlatko Krmpotic: Kikosi kitaimarika
Kagere bado yupo yupo sana Msimbazi