Mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Misri Mohamed Salah Ghaly, amerejeshwa nchini Italia kwa mara nyingine tena baada ya makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa klabu yake ya Chelsea pamoja na AS Roma.

Mo Salah aliyesajiliwa na Chelsea mwaka 2014 akitokea FC Basel ya nchini Uswiz mwezi Januari, alipelekwa kwa mkopo kwenye klabu ya Fiorentina, kufuatia nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha The Blues kuwa finyu dhidi yake.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23, amekubali kurejea katika ligi ya Sirie A, na atakuwa na klabu ya As Roma kwa makubaliano ya usajili wa mkopo wa muda mrefu ambao utaishia mwishoni mwa msimu huu.

Chelsea wamefikia hatua ya kumrejesha Salah nchini Italia, baada ya kuona bado wanakabiliwa na mazingira magumu ya kumtumia mara kwa mara katika kikosi chao cha kwanza, hivyo wanaamini kuelekea kwake nchini Italia kutaendelea kumlindia kipaji chake.

Hata hivyo, Salah ameonyesha kuipokea vizuri hatua ya kurejehswa nchini Italia, ambapo saa kadhaa baada ya kukamilisha usajili wake wa mkopo alifanyiwa mahojiano katika kituo cha televisheni cha AS Roma na alisema ni faraja kubwa kuendelea kuwepo katika ligi ya Sirie A.

Amesema jukumu lake kubwa kwa sasa ni kuhakikisha anasaidiana na wachezaji wengine klabuni hapo, ili kufikia lengo la kuiwezesha AS Roma kutwaa ubingwa wa Sirie A, pamoja na kufanya vyema kwenye michuano ya barani Ulaya.

Msimu uliopita kuanzia mwezi Januari, Mohamed Salah akiwa na klabu ya Fiorentina alifanikiwa kucheza michezo 26 ya ligi ya nchini Italia na kufunga mabao 9.

Video: ‘Empire’ Yaachia Trailer Ya Msimu Wa Pili, Ni Zaidi Ya Vita Ya Familia
Thierry Henry: Arsenal Bingwa 2015-16