Wakati tetesi zikisema huenda Uongozi wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Simba SC ukamtimua kocha mkuu Didier Gomes, sababu kadhaa zinatajwa kama sehemu ya kutoa msukumo wa kufanywa kwa maamuzi ya kuondoka kwake klabu hapo.
Tetesi za kutimuliwa kwa kocha huyo kutoka nchini Ufaransa zilianza kuchukua nafasi jana Jumatatu (Oktoba 25), kufuatia kikosi cha Simba SC kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa kufungwa mabao 3-1 dhidi ya Mabingwa wa Botswana Jwaneng Galaxy.
Simba SC imetolewa kwenye michuano hiyo kwa faida ya mabao ya ugenini ya wapinzani wao, baada ya kupata mabao matatu jijini Dar es salaam, huku Mnyama akipata mabao mawili mjini Gaborone.
Sababu zinazotajwa huenda zikamtoa Gomes Simba SC ni;
- Kocha kuweka makundi/kuwepo mpasuko baina ya wachezaji
- Kocha kutowahitaji kabisa baadhi ya wachezaji katika Kikosi Cha Simba (Onyango, Mkude, Ajibu, Gadiel Michael na Kagere)
- Simba kwa sasa kuonekana inafunga mabao yasiyokuwa na mipango (Rejea michezo yao minne iliyopita)
- Kocha kuonekana ameishiwa mbinu.