Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wameahidi kumuonesha ushirikiano kazini Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, William Tate Ole Nasha na kuhakikisha Wizara inakuwa na matokeo chanya na yenye tija kwa Taifa.
Watumishi walibainisha hayo jijini Dodoma wakati wa mapokezi ya kiongozi huyo mpya aliyeteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 05 Disemba, 2020 na kuapishwa tarehe 09 Disemba 2020 katika viwanja vya Ikulu Jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi pamoja na watumishi wa Wizara walipokea Naibu Waziri, Ole Nasha alipokelewa na kumhakikishia ushikiano wa kazi ili kuiwezesha Wizara kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake. Prof. Kabudi alimhakikishia Naibu Waziri Ole Nasha ushirikiano wake binafsi na kutoka kwa watumishi wote na kwamba uwepo wake utaongeza nguvu za kuifikisha Wizara katika viwango vya juu kiutendaji.
Itakumbukwa kuwa Disemba 05, 2020 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alifanya uteuzi wa jumla ya Mawaziri 23 pamoja na Naibu Mawaziri 23