Uongozi wa klabu ya Ihefu FC, umetangaza dau kubwa kwa wachezaji wa timu hiyo, ili kufaniksha mpango wa kubaki Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu ujao wa 2021/22.

Ihefu FC inayoshiriki kwa mara ya kwanza Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara, imekua inajikongoja kwenye michezo ya ligi hiyo, na kwa sasa inashika nafasi ya 17 ikwa na alama 20.

Katibu Mkuu wa Ihefu Athuman Mndolwa amesema, wachezaji wameahidiwa donge nono endapo tu, watashinda kila mchezo wa ligi kuu, hadi mwishoni mwa msimu huu.

Amesema ahadi hiyo kwa wachezjai imetolewa ili kuongeza hamasa ya kupambana bila kuchoka katika kipindi hiki cha kuelekea michezo ya mwisho ya Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku malengo ni kusalia kwenye ligi hiyo.

“Uongozi umeongeza bonasi kwa wachezaji ikiwa ni njia kuamsha upya morali kwa wachezaji wetu, ambapo kila mchezo umetengewa fungu lake.” Amesema Mndolwa.

Licha ya kutotaja kiwango kilichoongezwa akidai ni siri ya ndani, Mndolwa amesema dau walilotenga kwa kila mchezo ni kubwa, ambalo kwa mchezaji wa Ligi Kuu ni kiwango bora ambacho kitachochea kujituma zaidi.

Ihefu FC itacheza dhidi ya Namungo FC April 08 ugenini Majaliwa Stadium, Ruangwa mkoani Lindi na kisha itarejea nyumbani Mbeya kucheza dhidi ya Mbeya City April 15.

Siwa: Ubingwa lazima 2020/21
Uuzaji wa pombe wapigwa marufuku Afrika Kusini