Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamanda Lazaro Mambosasa, amesema kuwa jeshi hilo litaendelea kuwakamata wale wote wanaofanya maombi kwaajiri ya mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa operesheni ya kuwakamata watu hao iko palepale na jeshi hilo litatoa idadi ya waliokamatwa pindi tu litakapomaliza jukumu hilo.

“Bado tunaendelea kuwakamata, operesheni inaendelea na tutatoa ripoti mara tu baada ya kumaliza tukio, lakini kwa sasa acha tuendelee kuwakama kwakuwa wamekaidi agizo la polisi la kuwataka wasifanye hivyo,”amesema Mambosasa

Hata hivyo, mapema hii leo asubuhi jeshi la Polisi limewakamata baadhi ya raia katika eneo la viwanja vya TIP Sinza jijini Dar es salaam, kwa tuhuma za kufanya mikutano isiyo rasmi kumuombea Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye amepigwa na risasi, kitendo ambacho walikipiga marufuku

Video: Makonda kuwakwamua watumishi wa umma jijini Dar
Dkt. Shein kuongoza Kikao cha Kamati Kuu CCM