Mamia ya watanzania wamejitokeza katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) kuaga mwili wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini Ali Mufuruki, leo Desemba 10, 2019.

Mwili wa Mufuruki uliwasili nchini jana jioni ukitokea Afrika kusini, baada ya kuagwa leo anazikwa katika makaburi ya kisutu jijini Dar es salaam.

Mufuruki amefariki Dunia usiku wa kuamkia Jumapili ya Disemba 08, 2019 akiwa Afrika Kusini, ambapo alikuwa akipatiwa matibabu ya maradhi yaliyokuwa yakimkabili katika Hospitali ya Morningside.

waombolezaji waliofika mapemaleo asubuhi kuaga mwili huo wameungana na viongozi mbalimbali, wastaafu na wafanyabiashara.

Miongoni mwa viongozi waliofika ni Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu (uwekezaji), Angela Kairuki, Waziri Mkuu msaafu, Joseph Warioba na aliyekuwa Waziri wa viwanda na biashara , Charles Mwijage.

Wengine ni Mbunge wa Muleba kusini, Prof. Anna Tibaijuka, katibu mkuu msaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana, naibu katibu mkuu ofisi ya Makamu wa Rais (muungano na mazingira) Joseph Sokoine na Mkurugrnzi wa taasisi ya Mwalimu Nyerere Joseph Butiku.

Gereza la Butimba laanza kuachia huru wafungwa
Video: Pazia lafunguliwa, Mufti apiga marufuku madufu moto

Comments

comments