Mahujaji 717 wanaripotiwa kufa na wengine 816 wamejeruhiwa baada ya kutokea makanyagano karibu na mji mtakatifu wa Makka, Saudi Arabia.

Watu hao waliokuwa wamefika katika eneo hilo kutoka sehemu mbalimbali duniani kwa lengo la kuhiji ili kutekeleza moja kati ya nguzo muhimu ya Imani ya Kiislamu, ni kati ya mahujaji 2,000,000 waliohudhuria hija mwaka huu.

Msemaji wa Baraza la Taasisi na Jumuiya za Kiislamu nchini, Shekhe Rajabu Katimba alisema kuwa watanzania 1,500 walienda Makka kuhiji mwaka lakini hakuna taarifa rasmi za kifo cha mtanzania. Taarifa ya msemaji huyo inakuja wakati ambapo kuna tetesi kuwa mtanzania mmoja alifariki katika tukio hilo.

Historia inaoenesha kuwa haya ni maafa makubwa kuwahi kutokea katika siku kuu ya Eid El Hajji tangu miaka 25 iliyopita. Kwa mujibu wa BBC, taarifa zilizotolewa na Kurugenzi ya Wizara ya Usalama wa Raia zinaeleza kuwa makanyagano yalitokea baada ya mahujaji kuongezeka ghafla wakati wakielekea kwenye mnara

CCM, Ukawa Wairuka MCT Kuhusu Mdahalo
Chris Brown Kuzuiwa Kuingia Australia Kisa Rihanna