Watu milioni tano na laki sita wametakiwa kuhama jimbo la Florida nchini Marekani kupisha kimbunga cha Hurricane Irma kinachoishambulia Cuba hivi sasa.

Idadi hiyo ni asilimia 25 ya wakaazi wa jimbo la Florida ambao wametakiwa kuhama kunusuru maisha yao baada ya watu zaidi ya 20 kuripotiwa kufariki katika eneo la Caribbean.

Kimbunga hicho cha Irma kilishambulia katika maeneo ya Camaguey Archipelago siku ya Ijumaa, hali inayotishia pia maeneo ya miji ya pwani hiyo na vijiji vya jirani.

Kwa mujibu wa kitengo maalum cha kushughulikia majanga ya kimbunga nchini Marekani, usiku wa kuamkia leo kimbunga cha Irma chenye mwendokasi wa kilometa 257 kwa saa kilitishia maeneo hayo.

Tangu kimbunga hicho kianze kuitikisa Marekani, baadhi ya maeneo yamekosa umeme na mawasiliano na maeneo ambayo yamepata changamoto zaidi ni miji ambayo iko nje ya maeneo ya majimbo husika.

 

 

Video: Hii ni laana na unyama kuhujumu uchumi wa nchi- Dkt. Mpango
LIVE BREAKING: Serikali ikipokea taarifa madini yaliyozuiwa uwanja wa ndege DSM