Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki Jinai, Balozi Ombeni Sefue amesema Wananchi wamekuwa wakilawalamikia Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya, kwa kuwakamata hata kwa sababu zisizo na mashiko.

Balozi Sefue ameyasema hayo hii leo Julai 20, 2023 katika Kikao cha Wajumbe wa Tume ya haki jinai, DPC na Wahariri wa Vyombo vya Habari Ikulu jijini Dar es Salaam.

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki Jinai, Balozi Ombeni Sefue.

Amesema, “ni kweli Wananchi wamelalamika sana na niwaambie ukweli tu kuna mahali Mtu kasema kwamba ‘DC akimmezea mate Girlfriend wako, anakusweka ndani Ijumaa hutoki mpaka Jumatatu.”

Aisha ameongeza kuwa, “sasa tunachosema yale Mamlaka waliyopewa Ma-RC na Ma-DC yalikuwa na sababu tatizo sio wao kuwa na Mamlaka tatizo yanatumika vibaya.”

Ajali ya Ndege: Marubani JWTZ wanusurika kifo Bukoba
Watuhumiwa wanafurahia kubaki Mahabusu - Feleshi