Mamlaka ya hali ya hewa imetoa tahadhari ya kubwa kwa wakazi wa ukanda wa pwani kuwa kutakuwepo na upepo mkali na mawimbi makubwa katika maeneo ya bahari ya Hindi.
Aidha, katika Maeneo yanayotarajiwa kukumbwa na hali hiyo ni pamoja na mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Katika taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo, imesema kuwa kunatarjiwa kuwepo na upepo mkali wa kasi ya kilomita 40 kwa saa na mawimbi yanayozidi mita 2 baharini hivyo watumiaji wote wa bahari wametakiwa kuchukua tahadhari kubwa.
Hata hivyo, hali hiyo inasababishwa na msukumo wa upepo wa kusi unaotokana na kuimarika kwa mgandamizo mkubwa wa hewa katika ukanda pwani hivyo kusababisha hali hiyo kutkea.