Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini imetoa tahadhari na angalizo kwa wananchi kutokana na vipindi vifupi vya mvua kubwa vinavyotarajiwa katika baadhi ya maeneo ya nchi yetu.

Ambapo mvua kubwa zinatarajiwa kunyesha katika maeneo ya Dar es salaam, Pwani, Lindi Mtwara, Singida, Dodoma, Morogoro, Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya, Songwe, Kilimanjaro, Manyara na Arusha.

Pia imeelezwa kuwepo kwa upepo wa Pwani unaotarajiwa kuvuma kwa kasi ya Km 30 kwa saa kutoka Kaskazini- Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kaskazini-Magharibi kwa Pwani ya Kusini.

Ambapo hali ya bahari inatarajiwa kuwa na mawimbi makubwa kiasi.

Matazamio kwa siku ya Jumatatu tarehe 12/03/2018, ni kuendelea kwa mvua kubwa kunyesha katika maeneo ya Ukanda wa Pwani ya Kusini na Nyanda za juu Kaskazini Mashariki.

 

Mkakati mzito wa kumng'oa Lissu TLS wasukwa
Mayweather kuzichapa ngumi na mateke, mkufunzi wake afunguka