Mamlaka ya maji mjini Tarime mkoani Mara imezindua Bodi ya maji yenye wajumbe 7 lengo likiwa kushirikiana na kutoa mawazo yao katika kushughulikia masuala ya maji ili kuhakikisha changamoto za maji zinatatuliwa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira katika Mji wa Tarime, Passian Martin almesema kuwa kwa miaka 6 mamlaka hiyo imekuwa ikifanya kazi bila bodi ya maji tangu mwaka 2012,nakwamba kuanzishwa kwake kutaongeza ufanisi wa kazi.
“Miaka yote hiyo mamlaka ilijiendesha yenyewe hivyo kukawa na changamoto katika maamuzi kwakuwa sasa tuna bodi mtatusaidia mambo mengi yanayohusu mamlaka ya maji,”amesema Martin.
Mwenyekiti wa Bodi ya Maji, Moses Marwa amewataja wajumbe wa bodi hiyo kuwa ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji, Elias Ntirihungwa, Calvin Mwasha ambaye ni Mganga Mkuu halmashauri hiyo, Rose Hosea, Agnes Mwita, Diwani wa Kata ya Nyandoto Sinda Sabega, na Kaimu Meneja wa mamlaka ya Maji Passian Martin.
Pia Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na Bodi wameunda kamati 2, Kamati ya fedha yenye wajumbe 4 Mwenyekiti akiwa ni Calvin Mwasha, Katibu Passian Martin, Elias Ntirihungwa na Rose Hosea, Kamati ya nidhamu yenye wajumbe 2 Mwenyekiti ni Sinda Sabega na Katibu Agnes Mwita.
Aidha, ameongeza kuwa bodi hiyo itakuwa inakutana mara moja kila baada ya miezi 3, kamati ya fedha itakutana mara moja kila mwezi na kamati ya nidhamu itakutana mara moja kila baada ya miezi 3 na punde kunapotokea dharura.
Kwa upande wake kaimu meneja wa maji ametaja majukumu ya Bodi ikiwa ni pamoja na kusimamia shughuli za mamlaka ya maji, kupitisha Bajeti ya fedha,kusimamia Vitabu vya kumbukumbu na uwasilishaji wa taarifa katika ngazi husika.
Naye Kaimu Mhandisi wa Maji halmashauri ya Mji Tarime, Laurent Mganga amesema kuwa kupitia Wizara ya maji iliwajulisha kuwa tayari kuna mradi mkubwa wa maji Tarime,hata hivyo hawajaelezwa mradi huo utaanza lini na wanapoulizia huambiwa waendelee kuwa wavumulivu.
-
Mrithi wa Nassari apatikana CCM
-
Dkt. Chegeni atimiza ahadi zake Busega
-
Video: Wakili Manyama amtaka CAG ajiuzulu