Beki wa kulia kutoka nchini Argentina na klabu ya Manchester City, Pablo Zabaleta yu njiani kuondoka Etihad Stadium, utakapofika wakati wa usajili wa majira ya joto.

Gazeti la Daily Mail limeripoti kwamba nyota huyo mwenye umri wa miaka 31 anawindwa na kocha wake wa zamani Roberto Mancini ambaye kwa sasa anainoa klabu ya Inter Milan.

Mkataba wa Zabaleta na klabu ya Man City umesaliwa na muda wa miezi 18.

Hata hivyo tatizo la majeraha ya goti ndiyo limekuwa kikwazo kwa Zabaleta kuonekana uwanjani mara kwa mara.

Kwa msimu huu Zabaleta ameitumia Man Citu katika michezo saba pekee.

 

Roberto Carlos Amkataa Neymar Real Madrid
Arsenal Wachokonoa Jambo Chelsea FC