Uongozi wa klabu ya Man City umedhamiria kumpigania mshambuliaji wake kutoka nchini Argentina Sergio Aguero, ili kuepuka adhabu ya kufungiwa zaidi ya michezo miwili, kufuatia kitendo cha kumpiga kiwiko beki wa West Ham Utd Winston Reid.

Man city wamejipanga kupambana na sakata hilo, kwa kuamini huenda kulikua na shinikizo la tukio hilo ambalo halikuonwa na muamuzi Andre Marriner ambaye alichezesha mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita.

Chama cha soka nchini England (FA) kilimfungulia mshataka Aguero na kumtaka awasilishe utetezi wake kabla ya saa kumi na mbili jioni hapo jana kwa saa za nchi hiyo.

Kamati ya nidhamu ya FA inatarajiwa kukutana wakati wowote kuanzia hii leo kupitia utetezi wa mshambuliaji huyo na kama haitoridhishwa na sababu zilizoainishwa, huenda ikamfungia michezo zaidi ya miwili.

Hata hivyo utetezi uliowasilsihwa na Aguero huko FA, inaamika umepewa baraka na uongozi wa Man City ambao umeanza kuonyesha kwa vitendo kumpigania ili aweze kuepuka adhabu inayomnyemelea.

Michezo ambayo huenda Aguero akaikosa kama atafungiwa ni dhidi ya Man Utd (Old Trafford – Septemba 10), Bournemouth (Etihad Stadium – Septemba 17) pamoja na mchezo wa kombe la ligi (EFL Cup) dhidi ya Swansea city utakaochezwa Septemba 21.

Gianluigi Buffon: Ninatamani Kucheza Klabu Moja Na Balotelli
Video: DC Mjema akabidhi daipa elfu 85,000 Hospitali ya Amana DSM