Nyota wawili wa klabu ya mpira ya Manchester City, David Silva na Vincent Kompany wamejengewa sanamu.

Masanamu ya wachezaji hao yanatarajiwa kuanikwa hadharani mwishoni mwa juma katika uwanja wa Etihad kabla ya mchezo kati ya Manchester City na Arsenal.

Inaelezwa kuwa, sanamu ya tatu ya Sergio Agüero itajengwa mwakani ili kuonyesha mchango wa klabu hiyo katika kuthamini mchango wa wachezaji hao.

Kompany aliondoka Man City mwaka 2019 na tayari alikuwa ameishindia makombe manne, mawili ya FA na manne ya EFL wakati Silva anatajwa kuwa moja ya wachezaji bora wa klabu hiyo.

Masanamu hayo yametengenezwa na Andy Scott ambaye kutokana na ugonjwa wa UVIKO-19 amekuwa akionana na nyota hao kwa njia ya mtandao pekee ‘online’.

Usajili DTB FC balaa tupu
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Augusti 24, 2021