Tayari klabu za ligi kuu ya Uingerza zimepiga kura na kukubaliana kuwa dirisha la usajili lifungwe kabla ya msimu kuanza mwaka ujao lakini baadhi ya klabu zikiwemo Manchester United na Manchester City zalipinga jambo hilo.

Kwa kawaida dirisha la usajili katika ligi kuu ya Uingereza huendelea kuwa wazi hadi tarehe 31 mwezi Agosti wakati ligi ikiwa imeanza na michezo kadhaa ikiwa tayari imechezwa.

Katika kura zilizopigwa vilabu 14 vikiwemo vilabu vikubwa kama Arsenal, Chelsea, Liverpool na Tottenham walipiga kura ya ndio kwamba dirisha hilo liwe linafungwa mapema kabla ligi kuu ya Uingereza haijaaanza.

Mahasimu wawili kutoka jiji la Manchester  walipinga jambo hilo wakitaka dirisha hilo la usajili kufungwa muda unaotumika siku zote ambapo huwa linafungwa huku ligi ikiwa imeanza.

Sio Man United tu na City wanaotaka lifungwe huku ligi ikiwa imeanza bali pia Watford, Swansea, Crystal Palace pia waliungana na City na United huku Burnley wakiwa hawajapiga kura kabisa.

Video: Chadema kuchangia damu nchi nzima
Fahamu chimbuko la wanawake kuvaa wigi