Manchester City leo imetoa tangazo la kuuza sehemu ya hisa za umiliki wa klabu hiyo kwa kampuni ya Kichina.

Mmiliki wa Manchester City Sheikh Mansour ameuza hisa 13% za umiliki wa wake kwa CFG kwenda kwa wawekezaji wa kichina – ambao wataingiza ndani ya kampuni kiasi cha $400m.

Biashara hii inakuja mwezi mmoja baada ya Raisi wa China kuitembelea Manchester City na alionekana akipiga selfie na mshambuliaji Sergio Aguero na waziri mkuu wa England, David Cameroon.

Dili ni ushahidi wa kiasi gani Premier League imekuwa sana katika miaka ya karibuni, Mansour alilipa kiasi cha $400m kuimili kwa asilimia 100% mnamo mwaka 2009. Miaka sita baadae ameuza kiasi cha 13% kwa bei ile ile aliyoinunua klabu nzima.

Hata hivyo, kuna vitu kadhaa bado havipo wazi, ikiwemo ni kiasi gani kitawekezwa katika timu ya Man City tu.

TANGAZO LA MAN CITY

City Football Group (CFG) leo inatangaza kuunda ushirikiano wa kibiashara na taasisi inayojumuisha wawekezaji wa kichina ambao wanaongoza vyombo vya habari, burudani, michezo na internet – chini ya kampuni ya CMC (China Media Capital) Holdings. Makubaliano ya kibiashara ya baina ya CFG na CMC Holdings na CITIC Capital yatahusisha uwekezaji wa US$400 million ambao utahusisha uamishwaji wa hisa 13%to za City Football Group kuwa chini ya CMC.

Biashara hii itaifanya kampuni kuwa na thamani ya US$3 billion.”

Safari Za Barani Afrika Kumtimua Ronaldo Mjini Madrid
Rais Asitisha Mchezo Wa Soka Dakika Ya 63