Uongozi wa klabu ya Man City umeripotiwa kuanza mazungumzo na klabu ya Wolfsburg ili kukamilisha azma ya kumsajili kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji, Kevin De Bruyne.

Awali, Man City walionyesha nia ya kutaka kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, kwa ada ya paund milioni 40, lakini mambo yalikwenda mrama kwa kiasi hicho cha pesa kukataliwa.

Kwa sasa Man City wanajipanga kuanza mazungumzo ya usajili wa De Bruyne, huku wakiripotiwa kuwa tayari kutoa kiasi cha paund milioni 50, kwa ajili ya kiungo huyo ambaye aliuzwa na Chelsea mwaka 2013 kwa ada ya paund milioni 18.

Thamani ya mchezaji huyo imeonekana kupanda kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha katika miaka miwili aliyoitumikia klabu ya Wolfsburg ambayo msimu ujao itashiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya kumaliza katika nafasi ya pili kwenye masimamo wa ligi ya nchini Ujerumani msimu uliopita.

Klabu bingwa nchini Ufaransa Paris Saint-Germain pamoja na ile ya Italia Juventus nazo zimeoshaonyesha nia ya kutaka kumsajili De Bruyne, hatua ambayo pia inatajwa kuongeza thamani ya usajili wake.

Mbowe Azungumzia Mgombea Urais Ukawa
Liverpool Wamnasa Benteke