Klabu ya Manchester City, imeripotiwa kukubali kutoa kiasi cha paund milion 54 kwa ajili ya kumsajili kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji pamoja na klabu ya VFL Wolfsburg ya nchini Ujerumani Kevin De Bruyne.

Man City wamebainika kufikia uamuzi wa kulipa kiasi hicho cha pesa kufutia mazungumzo yaliyochukua majuma kadhaa dhidi ya viongozi wa VFL Wolfsburg ambao walionyesha msimamo wa kutokuwa tayari kumuuza kiungo huyo chini ya paund million 50.

Baadhi ya vyombo vya habari nchini Ujerumani viliripoti taarifa hizo dakika chache baada ya makubaliano kufanyika, na huenda Kevin De Bruyne akaelekea nchini England wakati wowote kuanzia sasa tayari kwa kufanyiwa vipimo vya afya.

De Bruyne aliwavutia viongozi wa klabu ya Man City kufutia uwezo mkubwa aliouonyesha msimu uliopita ambao ulichangia kuifikisha VFL Wolfsburg katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ya nchini Ujerumani, kabla ya kutwaa ubingwa wa kombe la chama cha soka nchini humo mwishoni mwa msimu uliopita.

Alifanikiwa kufunga magoli 10 katika michezo ya 34 ya msimu uliopita aliyofanikiwa kucheza huku akitoa pasi za mwisho 20 zilizozaa magoli yaliyofungwa na wachezaji wengine wa VFL Wolfsburg.

Mipango ya kutarajia kuihama VFL Wolfsburg, imekuja kwa Kevin De Bruyne, baada ya kushuhudia usajili wake akitokea Chelsea ukidumu kwa miezi 20 ambayo ni sawa na mwaka mmoja na miezi minane.

VFL Wolfsburg, walimsajili Kevin De Bruyne, kwa ada ya paund million 20 akitokea Stamford Bridge ambako alikosa nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Bodi Ya Ligi Yaanika Hadharani Ratiba Ya FDL
Twiga Yajifua Zanzibar