Klabu ya Man City imeliweka jina la Thorgan Hazard katika orodha ya wachezaji wanaolengwa kusajiliwa klabu hapo katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.

Tayari wamepiga hodi katika klabu anayochezea Hazard ya Borussia Monchengladbach inayoshiriki Bundesliga.

Kwa mujibu wa Daily Mail, Spurs inapambana na klabu nyingine zinazowania saini ya kiungo huyo zikiwemo Liverpool, Westham na Swansea  ambazo zote zinapigana vikumbo.

Lakini City imetajwa kuwa katika mkakati mzuri wa kumrudisha Hazard katika Ligi ya premier akitokea katika klabu yake ya sasa ya Borussia Monchengladbach ya nchini Ujerumani.

Hazard aliondoka katika Ligi Kuu ya England katika usajili wa majira ya kiangazi kwa dau la paundi mil. 5.9 na kutua katika Ligi ya Bundesliga.

Tangu atue katika Ligi ya Ujerumani, Hazard amekuwa katika kiwango bora miongoni mwa wachezaji wa idara yake na kuwavutia makocha wa ndani na nje na sasa anatarajiwa kutua premier.

Kiungo huyo raia wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 23 amekuwa mchezaji wa kwanza kuingia katika rada ya usajili wa Spurs inayopanga kupambana kwa ajili ya kuwa miongoni mwa timu tano za juu katika premier ifikapo mwishoni mwa msimu.

Klopp Aeleza Mikakati Ya Kusajili Mlinda Mlango Bora
Sepp Blatter Bado King'ang'anizi