Mabingwa wa Soka nchini England ‘Manchester City’ wanapanga kufanya mazungumzo na Mshambuliaji Erling Haaland ndani miezi  michache ijayo kwa ajili ya kumuongeza mkataba mpya kwa mujibu wa ripoti.

Haaland amebakiza miaka minne katika mkataba wake ambao alisaini wakati anajiunga akitokea Borussia Dortmund lakini mabosi wa klabu wameona umuhimu wa kumwongeza mwingine kutokana na mchango wake mkubwa Etihad.

Taarifa zimeripoti Haaland ataongezewa mshahara mnono kufikia Pauni 400,000 kwa juma na jambo hilo litakuwa pigo kwa Real Madrid ambayo ilihusishwa na Mshambuliaji huyo.

Madrid ilionyesha nia ya kumsajili Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 baada ya kumkosa Kylian Mbappe kutoka Paris Saint-Germain.

Licha ya Madrid kuonyesha nia ya kumsajili mwaka jana katika dirisha la usajili la kiangazi, Haaland alichagua Man City ambayo ilimnunua kwa Pauni 51 milioni.

Katika msimu wake wa kwanza akiwa City Haaland aliweka kambani mabao 5-2 katika mashindano yote.

Mikutano itumike kukitangaza Kiswahili - Dkt. Ndumbaro
Zuieni Rushwa kabla haijatokea - Simbachawene