Mabingwa wa soka nchini England Manchester City wanapata kigugumizi cha kumuuza mshambuliaji wao wa pembeni kutoka Ujerumani Leroy Aziz Sané, ambaye ameonyesha nia ya kujiunga na FC Bayern Munich.
Sane amebakiwa na mkataba wa mwaka mmoja, na bado ana changamoto ya kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester City chini ya meneja Pep Guardiola.
FC Bayern Munich nao wameonyesha nia ya kutaka kumrejesha nyumbani mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24, kwa kununua mkataba wake uliosaliwa na miezi 12.
Guardiola anatajwa kuwa kikwazo cha dili la mshambuliaji huyo kuondoka, huku akiamini bado anahitaji huduma yake katika mipango ya msimu ujao wa ligi, japo imeonekana hamtumii mara kwa mara.
Endapo Manchester City watadhihirisha kumuuza Sane, watahitaji kiasi cha Pauni milioni 35, kama ada ya uhamisho.
Tetesi zinasema tayari mshambuliaji huyo ameshafanya makubaliano binafsi na FC Baryern Munich, na kinachokwamisha ni maamuzi ya mwisho kutoka kwenye uongozi Manchester City.
Sane aliyejiunga na Manchester City mwaka 2016 akitokea Schalke 04, imeelezwa amekukubali mkataba wa miaka mitano wa kuwatumikia mabinga hao wa Ujerumani,
Sane hajacheza soka tangu alipopata majeraha ya goti, wakati wa mchezo wa ngao ya jamii (Community Shield) uliochezwa Agasti 2019.