Klabu ya Manchester City imepaa kilele mwa ligi kuu ya Uingereza baada ya kuifunga Watford mabao 6-0 katika mchezo uliopigwa leo katika uwanja wa Vicarage Road.

Sergio Aguero alikuwa wa kwanza kuipatia Manchester City bao la kwanza dakika ya 27 na muda mchache baadae kupachika bao la pili dakika ya 29 kabla ya mshambuliaji wakibrazil Gabriel Jesus kupachika bao la tatu dakika 37.

Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa Man City kuongoza mabao 3-0 na Watford walioonekana kuzidiwa zaidi hawakuonyesha tofauti yoyote katika kipindi cha pili kwani dakika ya 63 ya mchezo huo mlizi wa Man City alipachika bao la nne.

Zikiwa zimebaki dakika 9 tu mchezo huo kumalizika mshambuliaji wa Argentina Sergio Aguero alipiga hat-trick yake ya kwanza msimu huu akipiga bao la tano dakika ya 81.

Watford wakiwa wanatafuta bao la kufuta machozi muingereza Raheem Starlig aliwachambua mabeki wa Watford na  kuingia ndani ya eneo la hatari ambapo aliangushwa na muamuzi akaamuru ipigwe penati iliyopigwa na Starling mwenyewe aliyepachika bao la 6.

Kwa ushindi huo sasa Manchester City imekaa kileleni mwa ligi kuu baada yakufikisha pionti 13 ikiwa juu ya Manchester United wenye pointi 10 wakiwa wamecheza maichezo 4.

Nyumba ya Zitto Kabwe yateketea kwa moto
Hodgson aanza kwa kipigo Crystal Palace