Mwenyekiti wa klabu bingwa nchini Ujerumani FC Bayern Munich Uli Hoeness ametangaza rasmi kuiondoa klabu hiyo kwenye mchakato wa kumuwania mshambuliaji kutoka nchini Chile Alexis Sanchez.
FC Bayern Munich waliwahi kufanya mazungumzo na mshambuliaji huyo wa Arsenal kabla ya msimu wa 2016/17 haujafikia kikomo, hali ambayo ilikoleza taarifa za Sanchez kuondoka Emirates Stadium katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi.
“Hatuwezi kutengeneza kikosi kwa kutumia kiasi cha milioni 100 kwa mchezaji anaekaribia miaka 30,” Amesema Hoeness.
Kujiondoa kwa FC Bayern Munich kunaiacha klabu ya Man city katika mbio za kumuwania Sanchez ambaye bado yupo kwenye mazungumzo ya kusaini mkataba mpya na uongozi wa Arsenal.
Mkataba wa sasa wa Sanchez unatarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu wa 2017/18.