Klabu ya Man Utd imepata faida kubwa ya fedha tofauti na klabu nyingine duniani kwa kipindi cha msimu uliopita, hii ni kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na kampuni ukaguzi duniani (Deloitte).

Pamoja na kutokua na kiwango kizuri cha kusakata kabumbu, klabu hiyo imeishinda hata Real Madrid waliofanikiwa kutwaa ubingwa wa soka barani Ulaya msimu uliopita. Real Madrid pia wamekua wakifanya vizuri katika upande wa klabu za soka duniuani kwa miaka 11 iliyopita.

Ukijumlisha kipato cha timu ishirini bora kwa msimu wa 2015-2016 kimeongezeka kwa asilimia 12 na kufikia euro billioni 7.4, hatua ambayo haikuwahi kufikiwa hapo awali.

Hii ni mara ya kwanza kwa Man United kushikilia nafasi hiyo tangu msimu wa 2003-04.

Real Madrid wameshuka mpaka nafasi ya tatu wakiwaacha wapinzani wao wakubwa FC Barcelona katika nafasi ya pili.

Mabingwa wa Ujerumani FC Bayern Munich wapo nafasi ya nne huku matajiri wa jiji la Manchester (Man City), wakishika nafasi ya tano kwa kutengeneza Euro milioni 524 kwa msimu uliopita.

Hii ni mara ya kwanza kwa Man city kuingia katika nafasi hiyo.

 Orodha Ya Timu 10 Zilizoingiza Mapato Makubwa 2015-2016

1 Manchester United-689

2 Barcelona-620.2

3 Real Madrid-620.1

4 Bayern Munich-592

5 Manchester City-524.9

6 Paris St-Germain-520.9

7 Arsenal-468.5

8 Chelsea-447.4

9 Liverpool-403.8

10 Juventus-341.1

Maneno ya Mwijage kuelekea Tanzania ya viwanda
Jeshi la Gambia latoa tamko kwa majeshi yanayopanga kumng'oa Rais Jammeh