Mashetani Wekundu (Man Utd) wanaandaa ofa ya paundi milioni 155 kwa ajili ya kumnyakua nyota wa Juventus Paulo Dybala.

Mshambuliaji huyo raia wa Argentina alitupia mabao mawili kwenye ushindi wa 4-0 ambao mabingwa watetezi hao wa Sirie A, waliupata dhidi ya Torino mwishoni mwa juma lililopita,  huku gazeti la Sunday Mirror la nchini England likiripoti kuwa mabosi wa United wanajiandaa kuchuana vikali na Barcelona.

Juventus wamesisistiza kuwa Dybala mwenye umri wa miaka 23, hana kipengere cha ofa maalum ya kuuzwa kwenye mkataba wake, na ofa yoyote ambayo itazidi ile ya Paul Pogba basi watakubaliana nayo.

Hata hivyo bosi wa Juventus, Giuseppe Marotta amesema kuwa hatamzuia nyota huyo kuondoka.

Dybala amefunga magoli 12 kwenye mechi nane azlizoichezea Juventus msimu huu huku akiwa anaendelea kuimarika.

Maalim Seif aongoza jopo la viongozi Kenya kwa Lissu
Azam FC kuifuata Singida Utd kesho