Uongozi wa klabu ya Manchester United umekanusha taarifa za kuwa mbioni kumtimua meneja Jose Mourinho, kama baadhi ya vyombo vya habari nchini England vinavyoendelea kueleza.

Taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo hivyo zinaeleza kuwa, Mourinho huenda akatimuliwa baadae hii leo, endapo kikosi chake kitashindwa kupata ushindi dhidi ya Newcastle United kwenye mchezo wa ligi kuu ya nchini England.

Jana ijumaa taarifa hizo ziliibuliwa kwa wingi, lakini uongozi wa Man Utd ulikaa kimya mpaka mapema hii leo ulipotoa taarifa ya kukanusha kwa kueleza: “Hali ya klabu ni shwari, hakuna ukweli wa taarifa zinazoendelea kusambaa kwenye vyombo vya habari, tuna imani na Jose Mourinho, na tunamtakia kila la kheri kwenye mchezo wa leo.”

Mourinho amekua na wakati mgumu wa kupata ushindi siku za karibuni, baada ya kukishuhudia kikosi chake kikishindwa kuunguruma katika michezo minne iliyopita.

Mwishoni mwa juma lililopita, Man Utd walipoteza mbele ya West Ham Utd kwa kukubali kibano cha mabao matatu kwa moja, wakiwa uwanja wa ugenini London Stadium.

Mourinho alikua anapewa nafasi kubwa ya kuikomboa Man Utd, tangu alipoajiriwa klabuni hapo miaka miwili iliyopita akichukua nafasi ya Louis Van Gaal, lakini imekua tofauti.

Kwa msimu huu wa 2018/19 ameshapoteza michezo mitatu ya ligi kuu ya England na kutolewa kwenye mcihuano ya kombe la ligi (Carabao Cup) kw akufungwa na Derby County.

Michezo ya ligi aliyopoteza ni dhidi ya Brighton And Holve Albion, Tottenham Hotspurs na West Ham Utd.

Atiwa mbaroni kwa kujifanya daktari bingwa
Hatma ya De Bruyne mikono mwa madaktari