Meneja wa Manchester United Louis van Gaal hakutaka kujiuzulu siku ya Jumamosi, baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Southampton, licha ya taarifa kadhaa kudai hivyo. Van Gaal, 64, inadaiwa alimwambia makamu mwenyekiti wa Manchester United, Ed Woodward kuwa yuko tayari kuacha kazi baada ya kufungwa 1-0 na Southampton.

Vyanzo kadhaa vimeiambia BBC Sport kuwa mazungumzo kama hayo hayakutokea. Van Gaal, ambaye jina lake halisi ni- Aloysius Paulus Maria “Louis” van Gaal- amerejea kwenye uwanja wa mazoezi wa United siku ya Jumanne wakati wanajiandaa kupambana na Derby County siku ya Ijumaa kwenye mchezo wa Kombe la FA.

Manchester United wanaendeleza msimamo wao wa kutozungumzia waziwazi hatma ya Van Gaal.

Stewart Aizungumzia Michuano Ya Zambia
Baba Samatta Azungumza Neno La Faraja Kuhusu Mwanae

Comments

comments