Hatimaye beki wa pembeni kutoka nchini Brazil, Rafael da Silva amekamilisha safari wa kuihama klabu ya Man Utd na kuelekea nchini Ufaransa kujiunga na Olympic Lyon.

Mipango ya usajili wa beki huyo mwenye umri wa miaka 25 ilikamilishwa jana jioni na tayari ameshasainishwa mkataba wa miaka minne wa kuitumikia klabu hiyo ya mjini Lyon.

Rafael, ameondoka Man Utd baada ya kushindwa kumridhisha meneja wa sasa wa klabu hiyo Louis van Gaal, na msimu uliopita alipata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza mara sita, tofauti na ilivyokua wakati wa utawala wa Sir Alex Ferguson.

Mara baada ya kukamilisha usajili wa kujiunga na Olympic Lyon, Rafael aliwashukuru mashabiki, wachezaji pamoja na uongozi wa Man Utd kwa ukarumu waliomuonyesha wakati wote alipokuwa klabu hapo tangu mwaka 2008.

Rafael aliekea barani Ulaya sambamba na pacha wake Fábio Pereira da Silva mwaka 2008 wakitokea nchini kwao Brazil kwenye kituo cha kulea na kuendeleza vipaji kinachomilikiwa na klabu ya Fluminense.

Chadema wawakabidhi Jahazi Lowassa na Juma Duni, wabadili jina la ‘Safari ya Matumaini’
Benitez Azifanyia Kauzibe Man Utd, Arsenal